HATUA 6 RAHISI ZA KUWA BORA KULIKO ULIVYOKUWA JANA

 

·         Jitambue (self awareness)

Tenga muda kila siku kujiangalia ndani yako tambua mawazo yako hisia zako na namna unavyoitikia mambo.

Kuandika au kutafakarikimyakimya hukusaidia kuanza safari ya kujijenga kwa uelewa.

 

·         Jenga uhusiano wako wa Mungu/chanzo (Hatua ya kiroho)

Tenga muda wa sala kutafakariau shukurani kila siku

Unganisha moyo wako na chanzo cha uhai.Roho ikipata amani mabadiliko ya kweli huanza kuonekana kwenye Maisha yako.

 

SSOMA PIA:Unakunywa maji vizuri? fahamu faida unazokosa ukipuuza hii tabia.

·         Jiweke malengo madogo na halisi

Usijisumbue na mipango mikubwa isiyotekelezeka .anza na tabia ndogo kama kusoma kurasa chache ,kusali,kunywa maji ya kutosha,au kunyoosha mwili. Hatua ndogo ndogo hujenga Imani ya ndani.

 

·         Lisha akili yako kila siku

Chagua kile kinachoingia akilini mwako. Soma maandiko ya kukuinua ,sikiliza mafunzo chanya au tazama vitu vinavyokujenga kiakili na kimaadili.

 

·         Jizungushe na mazingira chanya

Watu unaokaa nao na maudhuiunayoyafuata vina nguvu kubwa.

Chagua mazingira yanayokutia moyo kukua siyo yanayokurudisha nyuma.

 

·         Jitunze kimwili

Mwili wako ni hekalu

Pata usingizi wa kutosha fanya mazoezi mepesi na kula chakula chenye uhai.

Afya njema huisaidia akili na roho kukua.

 

SSOMA PIA:jinsi ya kutrack simu iliyoibiwa au kupotea na kuipata kwa haraka

KUMBUKA

Kujiboresha siyo kuwa  mkamilifu,

Ni kuwa bora leo japo kwa uchache kuliko ulivyokuwa jana.

Usisahau kukomenti,na kushare ili wengine wajifunze.

Previous Post Next Post

Ad 2