Siri za kufanikiwa katika umri mdogo Anza leo,Badilisha kesho

Chini ya miaka 40 ni muda mzuri wa kuwekeza na kupata mafanikio kwani unakuwa na nguvu za kufanya mambo makubwa .Tumia mbinu hizi:


ANZA MAPEMA KUWEKA AKIBA NA KUWEKEZA

Usisubiri upate hela nyingi hata elfu tano  kila wiki ukiweka baada ya miaka 5 ni mtaji mkubwa. Wenye umri mdogo wana faida ya  kuwa matajiri kama watawekeza mapema. Usikubali muda upite bila kufanya kitu kikubwa.

 SOMA PIA:Wajue wadukuzi wenye nguvu zaidi waliotikisa Dunia kupitia intaneti

JIFUNZE SKILLS ZENYE THAMANI KUBWA

Badala ya kupoteza muda mwingi kwenye starehe jifunze skills zinazolipa kama vile:

·         Digital marketing

·         Public speaking

·         Na kutumia AI kutengeneza  content

·         Uuzaji<sales>

·         Social media management

Skill moja thamani inaweza kukupa kipato kikubwa kuliko degree ya kawaida.

JENGA  MTANDAO  MAPEMA <NETWORKING>

Marafiki zako wa sasa ni wateja au waajiri wa kesho. Kuwa karibu na watu wenye ndoto kubwa kuliko wewe  watakubeba juu.epuka kuwa na watu wa kawaida kwenye circle yako.

EPUKA MADENI YA KIJINGANA STAREHE.

Usikimbilie mikopo ya simu za gharama kubwa wakati hazikuingizi kitu mavazi,au lifestyle. Ukiwa mdogo focus ya kwanza ni kujenga mtaji na biashara kubwa si kuonesha Maisha ya kifahari.

TAFUTA MWALIMU AU MENTOR

Tafuta mtu ambaye atakusimamia njia unayopita. Kila aliyeweza  kufanikiwa ana mtu ambaye alimpatia mwongozo wa kufanya. Usipoteze miaka 10 ukijaribu kila kitu tafuta mtu akupe short cut za kweli.

TENGENEZA VYANZO VINGI VYA MAPATO

Usitegemee ajira, kazi au biashara moja uhuru wa kifedha utapata ukiwa na vyanzo vingi. Hata bahari inakuwa na maji muda wote kwani ina mifereji mingi ya moto inayoingiza maji. Ndivyo ilivyo utafanikiwa kwa kufanya hivyo. Kila chanzo kidogo kinajenga nguvu kubwa.

WEKEZA KWENYE AFYA NA NIDHAMU

Mafanikio makubwa yanahitajimwili na akili yenye nguvu,mazoezi,usingiziwa kutosha  na kuepuka ulevi/ulegevu ni capital kubwa Zaidi kuliko pesa.

Ukijenga nidhamu ukiwa mdogo mafanikio yatakuwa matokeo ya lazima.

Wengi wanadhani mafanikio ni ya yawazee, lakini ukweli ni huu ukiwa kijana  una advantage kubwa  kuliko mtu yeyote.

Hizi ndizo mbinu zinazokufanya ufanikiwe ukiwa bado mdogo kuna ambazo tayari unazitumia au  ni jambo gani ambalombado unahitaji usimamizi  kati ya haya?

Niandikie hapo chini kwenye comment ili niweze kukusaidia.

Share ujumbe huu kwa watu wengine ili kuhamasisha mafanikio.

 

Previous Post Next Post

Ad 1

Ad 2